Makocha Wageni Wajaa Tanzania

Una Majina mengi sana huu Mchezo.Wengine tunauita Soka,Kandanda,Kabumbu nk.Lakini wewe tambua ni Mchezo wa Mpira wa Miguu,Mchezo ambao una matumizi makubwa ya Fedha.

Una Majina mengi sana huu Mchezo.Wengine tunauita Soka,Kandanda,Kabumbu nk.Lakini wewe tambua ni Mchezo wa Mpira wa Miguu,Mchezo ambao una matumizi makubwa ya Fedha.

Katika kuhakikisha Mchezo huu unasonga mbele zaidi,ni lazima kwa upande wa Kifedha Timu iwe imejipanga ipasavyo kisawasawa.Pesa itatumika kila Eneo.Kusajili Wachezaji,Kuajiri Makocha,Kuajiri Madaktari wa Timu,Kuajiri Ma Afisa Habari wa Timu nk.

Kama ilivyo sehemu nyingine Duniani,Nchini Tanzania nako hatuko nyuma katika Kulisakata Soka.Septemba 25 mwaka 2021,Ufunguzi wa Ligi Kuu ulifanyika kwa Mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa(Uwanja wa Taifa).Mchezo uliowakutanisha Timu kubwa zenye Mashabiki Wengi zaidi Timu za Yanga na Simba.Ambapo Yanga ilishinda kwa ushindi wa 1-0.Ikiashiria rasmi kufunguliwa kwa Msimu mpya wa Ligi 2021/2022.

Ligi hii kuu ya Soka Tanzania Bara,ni moja ya Ligi kubwa sana kwa sasa Barani Afrika.Msimu wa mwaka 2020/2021 ilichukua nafasi ya Nane (8) miongoni mwa Ligi Bora Afrika na Nafasi ya Sabini na Moja(71) Duniani kwa ubora.Imekuwa Ligi pendwa sana kwa sasa kwa Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Na imeonyesha kuwavutia Wachezaji wengi wa Kigeni kuja kucheza Soka Tanzania. Makocha wengi kwa sasa hawavungi kuja Tanzania kufundisha,pindi wanapofuatwa au hata wao wenyewe huomba Nafasi za kuja kufufundisha Kabumbu Tanzania.Msimu huu wa 2021/2022 umekuwa Msimu wa Makocha wengi kuchangamkia ‘FURSA’Tanzania kwani Makocha wa Kigeni wamekuwa wengi mno.


Ligi hii Kuu Tanzania Bara,Msimu huu ina jumla ya Timu kumi na Sita(16), Timu Kumi(10) zina Makocha Wakigeni na Timu Sita pekee zina Makocha Wazawa(Watanzania).

Hii hapa Orodha ya hao Makocha Wa Kigeni na makocha Wazawa.

MAKOCHA WA KIGENI

1. Simba-Didier Gomez De Rosa(France)

2. Yanga-Nasreddin Mohammed Nabi(Tunisia/Ubeligiji)

3. Biashara-Patrick Odhiambo(Kenya)

4. Azam-George Lwandamina(Zambia)

5. Mbeya Kwanza-Haruna Harelimana(Burundi)

6. Kagera Sugar-Francis Baraza(Kenya)

7. Mtibwa Sugar-Joseph Omog(Cameroon)

8. Geita Gold-Ettiene Ndayiragije(Burundi)

9. Coastal Union-Melis Medo(USA)

10. Mbeya City-Mathias Rule(Uganda)

MAKOCHA WAZAWA

1. Polisi Tanzania-Malale Hamsini Keya(Tanzania)

2. Tanzania Prisons-Salum Mayanga(Tanzania)

3. Namungo-Hemed Suleiman ‘Morocco'(Tanzania)

4. KMC-John Simkoko(Tanzania)

5. Dodoma FC-Mbwana Makata(Tanzania)

6. Ruvu Shooting-Charles Boniface Mkwasa(Tanzania)

Hii ya kuwa na Idadi kubwa ya Makocha wageni katika ligi ya Tanzania Bara kuzidi idadi ya Makocha Wazawa,siyo jambo baya.Kwa upande wa pili yawapasa Makocha Wazawa nao kutoka Nje ya Mipaka ya Tanzania kwenda kusaka Malisho zaidi.Inasemwa Makocha wetu wazawa ni Waoga sana wa Kutoka.Huu ni Muda wao wa kuonyesha uwezo wao.Watanzania hatupaswi kuchukia hali hii bali Makocha wetu Wazawa waibebe kama Changamoto waifanyie kazi.

By Kione Hamis Mahuruku